Lugha za Kinuristani

Lugha za Kinuristani ni jina la kundi la lugha hai zinazotumika hasa katika Nuristani (Afghanistan mashariki) lakini pia Pakistan magharibi. Kundi hilo linaainishwa kama mojawapo kati ya yale ya lugha za Kihindi-Kiajemi, hivyo kati ya kundi kuu la lugha za Kihindi-Kiulaya. Wasemaji wanahesabika kuwa 130,000 hivi.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search